Your experience on this site will be improved by allowing cookies
Katika ulimwengu wa sasa unaoongozwa na kasi ya teknolojia, blockchain imeibuka kama moja ya nguzo kuu zinazobadilisha taswira ya biashara, huduma, na mifumo ya kijamii.
Lakini swali muhimu linabaki—je, jamii ya Kiswahili na watu wa mataifa mbalimbali wanaelewa teknolojia hii, na je, tumeiweka katika muktadha unaoeleweka kwa jamii yetu?
Kupitia tafsiri ya kipekee iliyobuniwa na Antony Mlelwa (Mkurugenzi wa DIENA), blockchain inaelezewa kwa Kiswahili kama:
“Blockchain ni teknolojia ya kidigitali inayowezesha mtu au taasisi kuunda, kutekeleza na kusimamia mawazo ya kibiashara au huduma kwa kutumia programu otomatiki (smart contracts) badala ya kutegemea watu wengi au taasisi za kati katika uendeshaji.”
Tafsiri hii inasisitiza kwamba blockchain ni nyenzo ya kutekeleza mawazo ya kidigitali bila vizuizi vya taasisi za kati.
Leo hii, mtu anaweza kuwa na wazo la kibiashara—iwe ni huduma ya kifedha, jukwaa la kijamii, au suluhisho la changamoto ya kijamii—na kulitekeleza kupitia smart contract inayokimbia kwenye blockchain.
Kwa msingi huo, blockchain si tu teknolojia ya nyuma ya pazia, bali ni jukwaa hai la utekelezaji wa mawazo ya kibunifu.
Ni muhimu kuelewa kuwa blockchain ni nyenzo tu.
Kuwa na uwezo wa kuwasilisha wazo kupitia blockchain hakumaanishi kuwa wazo hilo ni bora, halali au litafanikiwa.
Ubora, uhalisia, na thamani halisi ya wazo ndicho kipimo cha mafanikio.
Katika wazo la uwasilishaji wa wazo la kibunifu, linaweza kuwa zuri au baya au lisilofanikiwa.
Hivyo ni muhimu kuwafanya watu watambue kuwa blockchain ni nyenzo tu, lakini kudumu na kufanikiwa kwa wazo liliwasilishwa na kusimamiwa kupitia blockchain itategemea uhalisia wa wazo lenyewe.
Kwa msingi huo, hata scam na mawazo ya kitapeli yanaweza kujengwa kwenye blockchain.
— Antony Mlelwa, Mkurugenzi wa DIENA
Kwa hiyo, matumizi ya blockchain yanapaswa kuambatana na maadili, utafiti, na usimamizi wa kina wa ubunifu husika.
Katika DIENA, dhamira yetu si kuielimisha jamii ya Kiswahili pekee, bali tumejikita kutoa mafunzo kwa hadhira ya kimataifa—ikiwemo Afrika, Amerika Kusini, na maeneo mengine duniani.
Mafunzo yetu yanatolewa kwa lugha mbalimbali, yakilenga kuhakikisha kila mtu anaelewa na kutumia blockchain kwa usahihi.
Lugha na eneo havitupi mipaka—tunazivunja kupitia maarifa ya kisasa.
Ni wakati wa jamii ya kimataifa kufahamu kuwa blockchain si tu fursa, bali pia ni wajibu.
Tunahitaji kuelewa teknolojia hii kwa kina, kuitumia kwa weledi, na kuzingatia maadili tunapobuni na kutekeleza mawazo ndani yake.
Katika safari ya kuelekea uchumi wa kidigitali, blockchain ni injini yenye uwezo mkubwa—lakini mwelekeo wake unategemea mikono ya wale wanaoitumia.
Kama viongozi, wabunifu, wataalamu na raia wa kawaida, tunabeba dhamana ya kuhakikisha teknolojia hii haitumiwi tu kwa faida binafsi bali kwa maendeleo ya pamoja.
DIENA, chini ya uongozi wangu kama Antony Mlelwa, imejikita kuhakikisha kuwa jamii za ndani na kimataifa zinaelimishwa kuhusu blockchain kwa njia sahihi, wazi, na yenye maadili.
Tuendelee kujifunza, kushirikiana, na kusimamia teknolojia kwa hekima.
Blockchain si mwisho, ni mwanzo wa safari mpya.
0 comments